Klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani imemteua meneja, Jupp Heynckes kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti hadi mwisho wa msimu.
Bayern Munich imetangaza kwamba Jupp Heynckes atarejea klabuni hapo kama kocha mkuu hadi mwisho wa msimu kufuatia kufungashiwa virago aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Carlo Ancelotti.
Licha ya kuiongoza Bayern kwenye Ligi ya Bundesliga msimu uliopita, Ancelotti alifukuzwa mwishoni mwa mwezi Septemba baada ya klabu hiyo kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka timu ya Paris Saint-Germain ya nchini Italia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Taarifa zinaeleza kuwa Ancelotti alikosa ushirikiano kutoka kwa wachezaji muhimu wa kikosi hicho na kuwa sababu kubwa ya kufungwa kwake.
Heynckes mwenye umri wa miaka 72 aliweka historia kubwa katika mchezo wa soka akiwa Bayern nakutangaza kustaafu hatimae anarejea tena kuokoa jahazi la timu hiyo linaloonekana kwenda mrama.
No comments: