Diamond kuwaimbisha ‘Hallelujah’ Wazanzibar

Msanii wa muziki Diamond Platnumz anatarajiwa kuangusha bonge la show katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar katika kilele cha Mwenge wa Uhuru.


Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, zinaonyesha kuwa mkali huyo wa ‘Hallelujah’ atafanya tamasha hilo siku ya tarehe 14 Oktoba mwaka huu katika kilele cha shereza za mbio za Mwenge.
Diamond ataongozana na timu yake ikijuisha madansa wake pamoja na bendi yake ambayo amekuwa akifanya nayo kazi katika matamasha makumbwa.

No comments: