Catalonia itatangaza uhuru wake kutoka Uhispania siku chache zinazokuja, kiongozi wa eneo hilo ameiambia BBC.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ifanyike kura ya maoni siku ya Jumapili, Carles Puigdemont alisema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo.
Kwa upande wake mfalme wa Uhispnia Felipe VI, amasema kuwa waandalizi wa kura hiyo walikiuka sheria.
Maelfu ya watu kote eneo la Catalonia wamekuwa wakigoma kupinga ghasa za polisi wa Uhispania wakati wa kura, ambapo takribana watu 900 walijeruhwia.
Wakati ya kura hiyo takriban polisi 33 pia walijeruhiwa.
Wakati wa mahojiano na BBC rais wa Catalonia Carles Puigdemont, alisema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzo wa wiki ijayo.
Alipoulizwa kuhusu ni kipi atakifanya ikiwa serikali ya Uhispania itaingilia kati na kuchukua udhibiti wa serikali ya Catalonia, Bw Puigdemont alisema kuwa yatakuwa ni makosa ambayo yatabadilisha kila kitu.
Bwana Puigdemont alisema kuwa sasa hakuna mawasiliano kati ya serikali mjini Madrrid na utawala wake.
Alipinga taarifa ya tume ya ulaya ya siku ya Jumatatu kuwa kile kinachoendelea Catalonia ni masuala ya ndania ya Uhispania.
No comments: