Mchekeshaji na muigizaji kutoka Bongo, Idris Sultani amemu-wish happy birthday Diamond kwa njia ya utani kwa kumshauri kutumia condom.
Idris ameandika katika mtandao wake wa Instagram kwenda kwa hit maker wa ‘Hallelujah’ kutumia kondom ili aepuka kutoa shilingi elfu sabini kwa ajili ya kuhudumia mtoto wake.
Dear @diamondplatnumz nimekaa nikawaza sanaaa ila nimemaliza na jibu nimepata, kama kaka au mshikaji wako nimeona kuna vituo vingi sana vya watoto wasio na uwezo wa kujisomesha na hata chakula hakitoshi, nimeona kuna vijana wengi hawana ajira, nimeona kuna wengi hawajui watamkaje kesho. Kwa sasa wewe unaweza kuwasaidia sanaaa. Utakua unajiuliza hii 500 ya nini ila nimegundua nikikupa hii 500 ntakua nimeokoa maisha ya watu wengi sna.Hii 500 NUNUA CONDOM ILI HIZO ELF 70 TUWE TUNATOA MISAADA NA RAV 4 ZITAPELEKA MCHELE ORPHANAGE.Happy birthday bro.
No comments: