Mkuu wa idara ya Uenezi CHADEMA, Hemedi Ali amefunguka na kusema gari ambayo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alipewa na Bunge kwa ajili ya mizunguko mbalimbali ambayo pia ilikuwa akiitumia Nairobi kwenye matibabu ya Lissu imenyang'anywa na Bunge
Akiongea kutokea Nairobi, Hemedi Ali amesema kuwa haoni dhamira ya dhati ya Bunge hilo kusema lipo tayari kumtibu Tundu Lissu ikiwa wamepokonya gari ambayo Kiongozi wa Kambi rasmi Bungeni alikuwa akiitumia Nairobi kwenye matibabu ya Tundu Lissu.
Akizungumzia suala hilo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amedai kuwa hana na taarifa hizo, ndiyo kwanza anazisikia kutoka kwa mwandishi na alimtaka mwandishi amuulize huyo aliyetoa taarifa kama kweli ametumwa na Mbowe.
TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHIN
No comments: