Umoja wa Mataifa wapongeza Saudi Arabia kwa kuruhusu wanawake kuwa madereva

Katibu Mkuu António Guterres kupitia ukurasa wake wa Twitter amekaribisha hatua ya mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud kutoa agizo la kuondoa zuio hilo akisema ni hatua muhimu kwenye mwelekeo wa haki.

Idhaa ya Umoja wa Mataifa ilizungumza na Mohammad Naciri ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake UN Women katika nchi za kiarabu ili kupata maoni yake kuhusu hatua hiyo..

"Tunaona kama hatua ya kiashiria kutoka kwa ufalme wa Saudi Arabia kuelekea kwenye fursa zaidi ya haki kwa wanawake wa Saudia kwenye ufalme huu."

Amesema kwa wanawake nchini Saudi Arabia uamuzi huo ni mwendelezo wa hatua muhimu ambazo zimekuwa zikichukuliwa na ufalme wa nchi hiyo.

"Kwa kuteua wanawake wa Saudi katika bunge la Saudia au baraza la Shura na pia kupitisha sheria kuhusu ukatili wa kingono na hatua hii ya lengo inafungua milango zaidi kuelekea usawa kwa masuala ya wanawake."

No comments: