Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dr. Kizza Besigye, amekamatwa na polisi nchini humo kufuatia sakata la baadhi ya wabunge na wananchi nchini humo kupinga suala la ukomo wa urais.
Dr. Besigye amekamatwa leo mchana katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala, ambako alikuwa amekwenda kuhamasisha wafuasi wake dhidi ya kuondolewa kwa Ibara ya 102 (b) ya katiba ya nchi hiyo, ambayo inaweka kikomo cha umri wa urais akiwa na umri wa miaka 75.
Wakati wa tukio hilo Dr. Besigye alikataa kushuka kwenye gari yake alipoamrishwa na polisi, na kuwalazimu polisi hao kuliburuza gari hilo hadi kituo cha polisi na kulipaki, huku Kizza Besigye akiwa ndani ya gari.
Mbali na Dr. Besigye Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Fred Mukasa naye amekamatwa na polisi kufuata tukio hilo.
No comments: