Maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba ni mojawapo ya matatizo yanayolalamikiwa na kina mama wengi.Kuna matatizo mengi ambayo yanahusiana tu na mimba, hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba hali yoyote ambayo husababisha maumivu katika mgonjwa asiyekuwa na ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito, ingawaje historia na uchunguzi vinaweza kuwa tofauti.
Kwa asili kutathmini maumivu ya tumbo kwa mama mjamzito ina changamoto kwa sababu kichefuchefu, kutapika, na maumivu ya tumbo hujitokeza mara nyingi kwa wajawazito wengi . Mfuko wa uzazi unapotanuka unaweza kusukuma viungo vingine kando ndani ya tumbo, upungufu wa damu na leukocytosis ni kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa vya upungufu wa damu au maradhi. Mgonjwa ambaye mimba imetunga nje ya mfuko kipimo cha ultrasound kinaonyesha majimaji na uchafu ndani ya mfuko wa uzazi bila ushahidi wa mimba.
Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi inaweza kusababisha maumivu ya tumbo , ambayo huchukua muda wa siku 1- 2 na kiasi kidogo cha damu ukeni. Mara nyingi kiasi hiki ni kidogo na hutokea kati ya siku 6 -12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa , mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa anatarajiwa kuingia hedhi. Hivyo, wagonjwa mara nyingi hufanya makosa kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida.
Mimba iliyotunga nje ya mfuko ni tatizo linaloongoza kusababisha maumivu kwa kina mama wengi sehemu mbalimbali duniani. Tatizo hili linaweza kubainika kwa kutumia Ultrasounda na kipimo cha homoni HCG. Hata hivyo tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji.
Sababu nyingine ni kutoka kwa mimba. Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo vya kina mama katika nchi zinazoendelea.
Uvimbe kwenye mirija ya mayai(Ovarian cyst). Wakati mwingine uvimbe huu hupasuka au kujizungusha. Hata hivyo unaweza kupungua na usipopungua unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa ujauzito.
Sababu nyingine ni kujizungusha kwa mirija ya mayai(Ovarian torsion). Hii hujitokeza mara chache.
Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa mkubwa. Tatizo hili linaweza kusababisha ujauzito kutoka hasa katika miezi ya awali.
Kidole tumbo(appendicitis) hujitokeza kwa uwiano sawa kama wanawake ambao hawana ujauzito. Matibabu ya ugonjwa huu ni upasauji. Mara nyingi wanawake wengi hupata uchungu baada ya upasuaji.
Kutokana na mabadiliko ya homoni wanawake wengi hupata tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo. Tatizo hii huweza kugunduliwa kwa njia ya ultrasound.Matibabu hutegemea na dalili
.
Uvimbe(inflammation) kwenye mfuko wa nyongo ni tatizo la ghafla linalosababisha maumivu makali ambalo pia hujitokeza wakati wa mimba. Tatizo hili mara nyingi husababishwa na mawe kweny mfuko wa nyongo. Antibiotics hutumika katika matibabau ya uchongo huu.
Wanawake wengi wakati wa hujauzito hupata maambukizi kwenye njia ya mkonjo mara kwa mara. Hii ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza wakati huu wa mimba.
Sababu nyingine ya maumivu husababishwa na ROUND LIGAMENT. Ligament hii ndio inayoshikilia mfuko wa uzazi tumbo. Mfuko wa uzazi unavyozidi kukua, ligament hii huvutika na kusababaisha maumivu.
Dawa za maumivu husaidia kwa tatizo hili.
Ultrasound hutumika katika uchunguzi wa maumivu ya tumbo wakati wa ujauzito. Kongosho, mfuko wa nyongo na kidole tumbo vyote huonekana kwa mama mjamzito. Vipimo vinavyotumia mionzi viyumike tu pale inapohitajika kwa mama mjamzito.
No comments: