Kampeni ya stop filamu ‘fake’ za nje ya RC Makonda imezaa matunda – Rado

Msanii wa filamu Rado, ambaye ni mmoja kati ya wasanii ambao waliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika kampeni ya kupiga stop filamu ‘fake’ za nje kwa madai zimeliaribu soko la filamu za ndani, inadaiwa kufanikiwa.
Image result for rado picha
Muigizaji huyo amedai kwa sasa kuna mahitaji makubwa ya filamu za ndani kutoka na madai ya kupungua filamu za nje.
‘Kusema kweli hali imebadilika sasa, wasanii wamepata nguvu mpya ya kurudi kwenye filamu baada ya kali ya soko kulaa vizuri, ile kampeni ambayo tulifanya na RC Makonda imezaa matunda sana,” alisema Rado. “Kuna umeangalia sasa hivi kuna kampuni nyingi za filamu zinaanzishwa, hii ina maana kwamba hali imeanza kukaa vizuri tofauti na awali,”
Bongo5 bado inaendelea kufanya jitihada za kuzungumza na baadhi ya wasanii pamoja na wadau ambao waliipinga kampeni hiyo kwa madai haiwezi kuisaidia tasnia ya filamu.

No comments: