Tajiri wa PSG atangaza dau kununua penati za Neymar kwa Cavan


Mmiliki wa klabu ya Paris Saint-Germain bilionea Nasser Al-Khelaifa ameonyesha jeuri ya fedha kwa kumtangazia mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Edinson Cavani ofa ya Euro milioni moja aridhie kumwachia Neymar Jr jukumu la upigaji penati ndani ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa El PaĆ­s, Al-Khelaifa alifikia uamuzi huo ili kuondoa tofauti zilizojitokeza kati ya wachezaji hao muhimu ndani ya klabu hiyo inayoongoza kwa upachikaji mabao katika League 1 nchini Ufaransa.

Cavani ambaye mpaka sasa amepachika mabao 7 katika michezo 7 aliyocheza amekataa ofa hiyo yenye thamani ya paundi 880,00 nakusema pesa kwake sio tatizo bali anahitaji heshima ndani ya klabu hiyo.

Ugomvi huu wa Cavani na Neymar ulianza  kujitokeza mchezo wa Ligi pale wawili hao walipogombania kupiga penati dhidi ya Lyon.

Wakati Neymar alipotaka kupiga mkwaju wa penati ndipo Cavani alipochukua mpira na kumwambia hilo ni jukumu lake na kumfanya raia huyo wa Brazil kubaki na kinyongo.

Licha ya ushindi waliyoupata wa mabao 2-0 katika mchezo huo dhidi ya Lyon mshambuliaji wa huyo wa Uruguay, Cavani alikosa penati huku ikielezwa kuwa tayari, Neymar ameshaomba radhi kwa tukio lilojitokeza.

No comments: