Kutoa ni moyo na sio utajiri, rapper Pitbull ametumia ndege yake binafsi kubebea wangojwa wa Saratani ili awaletwe katika hospitali zingine kupata Matibabu ya Chemotherapy, baada ya visiwa kisiwa cha Puerto Rico kuathirika na kimbunga ‘Maria’ na kupelekea kukosa huduma muhimu.
Rapper huyo ameungana na mastaa kama Jennifer Lopez aliyechangia kiasi cha dola milioni moja kwa wahanga na msanii Daddy Yankee aliyetoa pesa , kwa kusaidia wangonjwa hao ili waweza kupata matibabu baada ya kimbunga Maria kuharibu miundombinu kama huduma za maji, umeme na mpaka sasa hospitali 11 tu kati ya 69 za kisiwa hicho ndio kuna umeme kitu ambacho kinahatarisha maisha ya wagonjwa.
Kwa mujibu wa New York Daily News, wamesema kuwa Pitbull alishukuru kwa kutimiza wajibu wake kama binadamu.”Thank God we’re blessed to help. Just doing my part,” amesema Pitbull.
Kimbunga Maria kimekuwa kikiandama sehemu kadhaa za Amerika Kaskazini kama vile Kisiwa cha Caribbean, Guadeloupe, Dominica, St Kitts, Nevis, Montserrat na Martinique.
No comments: