HAKIMU Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha, jana Ijumaa hata kabla wikiendi haijaanza alimwachia huru mwanachama tajiri wa Yanga, Yusuf ivManji, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka la kutumia dawa za kulevya.
“Kusema ukweli nimefarijika sana kwa Manji kuachiwa huru kwa sababu mimi ndiye niliyemuwekea dhamana,” alisema Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa mara baada ya Manji kutoka mahakamani hapo.
“Katika kipindi chote nilikuwa na wasiwasi kuwa pengine lolote linaweza kutokea, lakini nashukuru Mungu ameachiwa huru.”
Mkwasa aliyewasili mahakamani akiambatana na baadhi ya wanachama, viongozi na mashabiki wa klabu hiyo aliongeza: “Tunaomba aje uraiani, tushirikiane katika majukumu.”
Wakili wa Manji, Hajra Mungula alisema: “Hukumu imetolewa vizuri na kama kuna lolote litasemwa baadaye.”
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ameshindwa kumtia hatiani mshtakiwa hivyo anamuachia huru.
Katika kesi hiyo, Manji alidaiwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin. Akipitia baadhi ya ushahidi mahakamani hapo, Hakimu Mkeha alisema shahidi wa tatu ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha Bapumia (62) alidai anashangaa mtu mwenye umri mdogo kama Yusufali Manji (41) kuwa na vyuma vinne kwenye moyo.
Awali, Yusuf Manji alidai kuwa yeye ana matatizo ya moyo ya kurithi kutoka kwa babu zake ambao walikwishafariki kwa ugonjwa huo.
No comments: