Jeshi la Polisi mkoani Kagera limekamata magunia Hamsini na Saba ya bangi yaliyokuwa yamehifadhiwa katika ghala la mkulima mmoja katika kijiji cha Mkatoketoke kata ya Ntobeye wilayani Ngara.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, -Augustino Ollomi amethibitisha kukamatwa kwa magunia hayo ya bangi huku mkulima huyo akiendelea kushikiliwa na jeshi hilo.
Kukamatwa kwa magunia haya Hamsini na Saba ya bangi ni matokeo ya oparesheni iliyoanza Agosti 15 na 16 mwaka huu kwa ushirikiano wa mikoa mitatu ya Kagera,Geita na Kigoma ambapo kamanda Ollomi anaelezea mafanikio yake.
Kwa mujibu wa Kamanda Ollomi, oparesheni hiyo itakuwa ikifanyika mara kwa mara na hivyo kuwataka Wakazi wote wa mkoa wa Kagera kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi.
No comments: