Mara Ngapi Umeshindwa Kufanikiwa Kwa Sababu Hizi?

Image result for picha ZA HUZUNI
Ni mara ngapi umekuwa ukitaka kubadilisha hali fulani hivi kwenye maisha yako, lakini cha ajabu tena umekuwa ukikata tamaa kwa mara ya kwanza hasa pale unapokutana  na changamoto kwenye maisha yako?

Ni mara ngapi umekuwa ukijiwekea malengo yako na kusema lazima nitatimiza lengo hili, lakini kitu cha ajabu umekuwa ukiyasahau malengo hayo mara moja na tena umekuwa huyakumbuki kama vile hukuweka malengo kabisa?

Ni mara ngapi umekuwa ukitoka nje ya mstari wa malengo yako uliyojiwekea hasa kutokana na maoni au malengo ya watu waliokwambia kwamba huwezi kitu hiki na wewe kutokana na kuwasikiliza ukaacha kweli?

Ni mara ngapi umekuwa ukisema utaweka akiba, ambayo itakusaidia baadae kuwekeza kwenye maisha yako, lakini umekuwa hufanyi hivyo kutokana na sababu zako ambazo unazijua wewe?
Ni mara ngapi umekuwa ukitoa sana visingizio badala ya kutoa matokeo yanayotakiwa kutolewa? Umeshawahi kujiuliza hili? Kila kitu unakuwa umejipanga kama vile unataka kutoa sababu badala ya kutoa matokeo yanatakayokusaidia kwenye maisha?

Ni mara ngapi umekuwa ukiishi maisha chini ya kiwango, maisha ya kuhuzunika na kuacha kuchukua hatua sahihi ambazo hatua hizo zinaweza kukupeleka kwenye mafanikio yako makubwa uyatakayo?

Muda huu na wakati huu ulionao una mahusiano moja kwa moja na kesho yako ya mafanikio. Hivyo, jinsi ambavyo umekuwa ukiahirisha mambo na kusema utafanya hili na hufanyi, elewa kabisa ndivyo umekuwa ukijiangusha mwenyewe kwenye maisha yako.

Unatakiwa kuishi kwa nia moja na hamu kubwa ya kujitoa hadi kufikia mafanikio. Lakini kama kila mara unasema unafanya hili halafu hufanyi, utakuwa unajenga tabia ambayo moja kwa moja msingi wake mkubwa ni kukuangusha na si kufanikiwa.

Najua changamoto kweli zipo katika maisha, lakini changamoto hizo isiwe sababu kubwa ya wewe kuacha mipango yako kila mara na kutoka nje ya mstari. Wakati wa kufanya na kutimiza ndoto zako ni sasa, fanya kitu.

Usikubali kushindwa kwenye maisha yako kwa sababu ya kutokufanya, usikubali kushindwa eti kwa sababu kila mara unaahirisha. Chukua hatua sahihi za kubadili maisha yako ili ufikie mafanikio makubwa. 

No comments: