LWANDAMINA BILA TSHISHIMBI LEO


IMG-20170930-WA0002

Msimu wa 2016-17 moja ya muunganiko hatari eneo la kiungo kwenye ligi kuu Tanzania bara , ulikuwa muunganiko wa Thabani Kamusoko akicheza kama kiungo wa chini, Haruna Niyonzima akicheza juu na Donald Ngoma akimaliza juu kama deep playmaker. Kulia Saimoni Msuva na kushoto Deusi Kaseke au Mwashuiya. Muunganiko huu ulimfanya mpinzani yoyote yule kuivaa Yanga kwa mahesabu makali ili timu yake ipate njia ya kwenda mbele kwenye ' locks' hizo pia kujilinda kwenye ' flow' .

Haupo tena muunganiko huo; Msuva katimkia Ughaibuni, Haruna katua Simba , Kaseke Singida United na kwa mbali Ngoma kasi imepungua baada yakuwa majeruhi wa muda mrefu.

Kupotea kwa muunganiko huo sio mwisho wa utawala wa wanajangwani hao eneo la kiungo; mwanzoni mwa msimu huu wamemleta kiungo mkabaji toka Mbabane Swallows Pappy Kabamba Tshishimbi.

Katika mechi nne alizocheza, Tshishimbi pia alitengeneza pacha nzuri ya kiufundi na kiungo mwandamizi wa timu hiyo Thabani Kamusoko. Kiasilia Kamusoko ni box to box midfielder, kiungo anayeweza kuisaidia timu kwenye patterns zote za kushambulia na kujilinda. Muunganiko wao na Tshishimbi umeifanya Yanga kuwa imara sana eneo la kati pia kuilinda vyema safu yao ya ulinzi.

Kiufundi Tshishimbi na Kamusoko imekuwa rahisi sana kwao kuelewana mapema kutokana na aina zao za uchezaji. Wote wana uwezo wa kukaba na kuchezesha timu kwa mifumo yote . Wana nguvu, kasi , uwezo wa kutoa pasi nzuri, kubadili mifumo yote ya kushambulia na kujilinda , kutibua mipango ya wapinzani nakutoa msaada kwa wenzao kwenye marking. Hili limewafanya kutengeneza pacha kamili kwa haraka na kumpa ahueni Lwandamina.

Alipokosekana Kamusoko kwenye mechi mbili za mwisho dhidi ya Majimaji na Ndanda, uliona kabisa jinsi gani pacha hiyo ilivyokuwa muhimu kwenye timu hiyo. Leo Lwandamina anakwenda kumkosa Tshishimbi je atafanikiwa mbele ya viungo wenye kasi , nguvu na damu changa toka Mtibwa Sugar?

Naheshimu sana uwezo wa viungo wa Mtibwa kwenye mifumo yote ya kuijenga timu kushambulia pia kujilinda ndio maana mpaka leo timu yao inaongoza msimamo wa ligi.

Lwandamina ni mmoja wa waalimu wazuri sana kumsoma mpinzani wake kabla na wakati mechi ikiendelea . Anajua kabisa pengo la Tshishimbi kwenye kikosi chake ndio silaha ya wapinzani wake katika kujenga mashambulizi yao. Yanga ina kikosi kipana hili binafsi siamini kama ni tatizo na Mtibwa wasijidanganye hilo.

Lwandamina ana uwezo leo kumtumia Kelvin Yondani kama kiungo wa chini , nyuma wakasimama Nadir na Dante na juu ya Yondani akacheza Rafael Daudi katika mfumo wa 4-2-3-1. Yaani timu ikawa na ' double six ' eneo la kati. Mechi ya mzunguko wa pili msimu uliopita Lwandamina alimtumia pia Yondani kama kiungo wa kati dhidi ya Mtibwa kule Jamhuri Morogoro hivyo si jambo geni.

Lakini pia ana uwezo wa kuwapanga Juma Makapu na Rafael Daudi kati na kumuacha Yondani na Dante wakisimama nyuma yao kama walinzi wa kati . Back up ya eneo la kiungo akalijengea mfumo mbadala pembeni na kati juu. Hili anaweza kulifanya kwa kuanzisha viungo wenye kasi , nguvu na uwezo wa kuwaminya Mtibwa kwenye channels zote tatu wacheze chini ya mstari wa kati ( defensive ). Kuanza na Mwashiuya kushoto, Juma Mahadhi au Buswita kulia na Ajibu kati kama false nine akitengeneza triangular midfield na viungo wawili wa nyuma yake yaani Makapu na Daudi ni dhahiri kiungo cha Mtibwa na walinzi wake wa kati watarudi nyuma. Hili litawezekana endapo kasi ya kushambulia kwa upande wa Yanga itakuwepo. Chirwa acheze kama mshambuliaji wa kati.

Siamini kama kiungo cha Yanga kitapwaya leo. Gadiel Michael akicheza kama alivyocheza mechi ya kwanza na Lipuli akisaidia marking pande zote sioni pengo la Tshishimbi kuidhuru Yanga sema tu linaweza kuifanya Yanga leo kucheza mchezo wa kujilinda zaidi kuliko kufunguka. Hili wanajangwani walitegemee sana kulingana na aina ya kikosi na wachezaji wao.

No comments: