Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo Jumamosi Septemba 23, kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti hapa nchini.
Mabingwa watetezi Yanga SC itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na endapo watashinda basi watafikisha alama 8 na kuikamata Simba kwa pointi. Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo utaofanyika Uwanja wa Mwadui Complex.
Mchezo mwingine, utakutanisha timu za Majimaji itakayokuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Mechi zote hizo zitaanza saa 10:00 jioni.
Yanga itaendelea kumkosa mshambuliaji wake Amis Tambwe ambaye bado anasumbuliwa na majeruhi na anatarajiwa kuanza mazoezi siku ya Jumatatu.
Mtibwa Sugar bado inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 9 ilizovuna katika michezo yake 3 huku. Nafasi ya pili inashkiliwa na Simba yenye alaam 8 katika michezo yake 4.
No comments: