amoja na magonjwa ya moyo kuwa chanzo kikuu cha vifo vingi duniani kuna uwezekano mkubwa wa kuyaepuka au kuishi nayo salama kwa kubadili mfumo wa maisha tunayoishi.
Hizi ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kupunguza magonjwa haya:
- Punguza kiasi cha chumvi na sukari badala yake tumia viungo vingine vitakavyoongeza ladha kwenye chakula.
- Epuka uvutaji wa sigara na tumbaku ambazo uharibu moyo na mishipa ya damu kutokana na uwepo wa nikotini na carbonimonoxide kwenye moshi wake na kusababisha magonjwa haya,
- Fanya mazoezi mepesi na yenye mpangilio walau kwa dakika 30 kila siku kupumguza shinikizo la damu, mafuta na uzito kupita kiasi.
- Kula lishe bora yenye matunda, mboga za majani na nafaka.
- Epuka matumizi ya dawa na madawa ya asili bila mpangilio na maelekezo ya wataalamu wa afya.
- Pata usingizi wa kutosha kila siku na usilale kupita kiasi.
- Cheki afya yako mara kwa mara asa kupima shinikizo la damu, uzito, sukari na mafuta mwilini.
- Punguza mawazo, hasira na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.
- Kwa ambao tayari wana magonjwa haya watumie dawa kama walivyoelekezwa na daktari.
- Jifunze na fuatilia kuhusu mambo ambayo yanakuweka katika hatari ya magonjwa ya moyo, dalili zake na tiba.
No comments: