Dirisha lijaro la Usajili Balani Ulaya
Klabu ya Everton inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa inatarajia kufanya mkutano ambao utakuwa na lengo la kuzungumzia namna ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Paris St-Germain ‘PSG’, Edinson Cavani mwenye umri wa miaka 30 ambaye kwa sasa amekuwa katika mgogoro na mchezaji mwenzake Neymar. (TuttoMercatoWeb – in Italian).
Mkufunzi wa Manchester United, Jose Mourinho yuko tayari kuwaongezea kandarasi wachezaji wake, Marouane Fellaini mwenye umri wa miaka 29, na Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 19, kuendelea kusalia Old Trafford. (Independent)
Bosi wa Manchester City, Pep Guardiola amesisitiza kuwa mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling mwenye umri wa miaka 22, atasalia katika klabu hiyo licha ya kuivutia Arsenal.(London Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Manchester City, Kevin de Bruyne anajiandaa kwa mazungumzo ya kandarasi mpya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ana takriban miaka minne iliosalia katika kandarasi yake lakini meneja, Pep Guardiola anataka mchezaji huyo kusalia kwa kipindi kirefu.. (ESPN)
Philippe Coutinho amesisitiza wito wake wa kutaka kuhamia Barcelona na Liverpool inapanga kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 mnamo mwezi Januari. (Sport via Mirror)
Real Madrid inapanga kumununua kiungo wa kati wa PSG, Julian Draxler mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akihusishwa na uhamisho wa Arsenal.(Daily Star via Don Balon)
Manchester United na Chelsea wote wanamsaka mshambuliaji wa Genoa Pietro Pellegri, lakini klabu hiyo hautamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 chini ya dau la £40m. (Sun)
Mkufunzi wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amefutilia mbali shaka kuhusu hatma yake ya siku za usoni katika klabu hiyo (Daily Star)
Klabu ya Deportivo La Coruna ya nchini Hispania inahitaji huduma ya aliyekuwa kocha wa Crystal Palace, Frank de Boer .(Sun)
Newcastle United inajiandaa kuanzisha mazungumzo na meneja, Rafa Benitez kuhusu kuandikisha kandarasi mpya kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mkufunzi huyo na mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley(The Times – subscription required)
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal, Fran Merida mwenye umri wa miaka 27, ambaye anaichezea klabu ya Osasuna katika Ligi ya pili ya Uhispania anasakwa na klabu ya Leeds. (sun)
Paris St-Germain imekataa kumuongeza marupurupu ya kitita cha Euro milioni 100 mshambuliaji wake, Edinson Cavani mwenye umri wa miaka 30, kwa kumuachia Neymar kupiga penati . (Independent)
Laurent Koscielny mwenye umri wa miaka 32, anasema kuwa mchezaji mwenza wa Arsenal, Alexis Sanchez ameahidi kuichezea klabu hiyo baada ya jaribio lake la kutaka kuondoka kugonga mwamba (Daily Express)
Kiungo wa kati wa Watford Nathaniel Chalobah mwenye umri wa miaka 22, atalazimika kusubiri ili kucheza nchini Uingereza baada ya kupata jeraha la goti(Daily Mail)
Beki wa kulia wa Manchester City, Kyle Walker mwenye umri wa miaka 27, amesema kuwa anafuraha kuwa yuko timu moja na Sergio Aguero akidai kuwa ni vigumu kukabiliana na mchezaji huyo. (Guardian)
Uefa imeipatia rukhsa klabu ya Bayern Munich kumrudisha kipa aliyestaafu, Tom Starke mwenye umri wa miaka 36, katika kikosi cha Klabu bingwa baada ya kumpoteza nahodha Manuel anayeuguza jeraha (ESPN)
Kiungo wa kati wa Monaco, Youri Tielemans mwenye umri wa miaka 20, amesema kuwa alikaidi uhamisho wa kuelekea Arsenal mnamo mwezi Agosti kuhusu wasiwasi kwamba huenda akapewa muda mchache kuichezea timu hiyo.(Metro)
Crystal Palace itamkosa mshambulaiji wake Christian Benteke, mwenye umri wa miaka 26, kwa takriban wiki sita akiendelea kuuguza jereha lake la goti. (Daily Telegraph)
Leicester wamewasilisha ombi kwa Fifa kwa lengo la kukamilisha usajili wa Adrien Silva mwenye umri wa miaka 28, kwa dau la paundi milioni 25 baada ya usajili wake wa siku ya mwisho kuchelewa (Daily Telegraph)
No comments: