Msanii wa muziki Bongo, Dayna Nyange amemtaja Nikki wa Pili kama mtu aliyepelekea kuacha muziki wa rap na kuanza kuimba.
Muimbaji huyo amesema kuwa kipindi cha mwanzoni alikuwa na uwezo mzuri katika rap na kulikuwa na mipango ya kusaini B Hit’s ambapo mara nyingi alikuwa na AY kama mshauri wake lakini Nikki wa Pili alimueleza kwa wakati huo kurap kusingemuingiza fedha.
“Nakumbuka mwanzoni nilikuwa nipo vizuri hadi nilikuwa nisaini na wakina Hermy B, B Hit’s kipindi kile na wakina AY tulikuwa tupo pamoja na ninakumbuka kuna kipindi tulikuwa tumeshaanza kufanya kazi AY akawa ananisaidia baadhi ya vitu. Kipindi hicho mtu kama AY ananisikiliza na kuonyesha nguvu yake, najiona ukubwa wangu ulikuwa sehemu gani,” Dayna ameiambia Bongo5.
“Nikki wa Pili ndiye alinitoa katika rap na kunileta kwenye kuimba, aliniambia ‘Dayna acha kurap utakuwa hupati hela aisee!’, basi Nikki nakushukuru, nikaacha nikaamua kuwa muimbaji na sasa hivi nina tuzo BAE, AFRIMMA, so kila jambo lina wakati wake,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine msanii huyo hajamiss kurap kwani kuimba kumemfaa zaidi na kurap alikuwa anatumia muda mwingi na nguvu zaidi ukilinganisha na kuimba.
“Kwenye kurap unatumia maneno magumu misamiati mafumbo lakini Bongo Flava hutakiwi kutumia mafumbo, ukitumia mafumbo wimbo mzima unaweza ukajipa mtihani, watu wanataka kusikiliza kitu laini laini na chepesi,” amesema Dayna Nyange
No comments: