cavan aikataa ofa ya billionear wa PSG Al-Khalaifi

Image result for cavani
Baada Ya Mmiliki wa klabu ya PSG bilionea Al-Khelaifi amemtangazia Edinson Cavan ofa ya Euro milioni moja aridhie kumwachia Neymar Jr jukumu la upigaji penati ndani ya klabu hiyo. 


Al-Khelaifi alifikia uamuzi huo ili kuondoa tofauti hasi iliyopo kati ya wachezaji hao wandamizi wa klabu hiyo ya League 1 nchini Ufaransa. Pesa hizo ambazo sawa na paundi 880,00 zimekataliwa na Cavan nakusema pesa kwake sio tatizo bali anahitaji heshima ndani ya klabu hiyo. 


Ugomvi huu wa Cavan na Neymar ulianza kwenye mechi ya ligi pale wawili hao walipogombania kupiga penati dhidi ya Lyon. Neymar alitaka kupiga penati lakini Cavan aliuchukua mpira na kumwambia hilo ni jukumu lake na kumfanya raia huyo wa Brazil kubaki na kinyongo. Cavan alikosa penati hiyo ingawa PSG ilishinda 2-0.

No comments: