Baada ya Diamond Platnumz kuweka wazi kuwa amezaa mtoto na Hamisa Mobetto akiwa kwenye mahojiano na Leo Tena ya Clouds FM leo September 19, 2017 kisha Zari kumuonya kuwa asimjaribu ishu hiyo sasa imefika hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
RC Makonda ameandika kwenye Instagram yake akimwambia Zari kuwa ana uwezo mkubwa wa kupita kwenye dhoruba na akaendelea kubaki imara na kuendelea kupata heshima kutoka kwa familia yake.
RC Makonda kaandika>>>”Thamani yako kwangu bado ni kubwa sana, kwani uwezo wako wa kupita kwenye dhoruba na ukabaki imara na familia yako unaendelea kukupa heshima.”
No comments: