Yanga ipo kwenye mchakato wa kukarabati uwanja wake wa Kaunda ambao utatumika kwa mazoezi ya timu za vijana na wakubwa pamoja na mechi za kirafiki. Katika ujenzi huo Yanga ilitangaza nafasi kwa mashabiki kuweza kuchangia chochote ikiwemo vifusi ambapo jambo hilo limepokelewa kwa nguvu.
Klabu hiyo imethibitisha kuendelea kupokea michango kutoka kwa wanachama wake mbalimbali. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa picha (Instagram) timu hiyo imewashukuru mashabiki ambao tayari wameshawasilisha michango yao.
Moja ya vikundi maarufu ambavyo vimejitolea kusaidia klabu yao ni Yanga Damu Original ambao wamepewa cheti cha shukrani na klabu ikiwa ni sehemu ya kuheshimu mchango ambao wameutoa.
Yanga itashuka dimbani leo jioni kuivaa KMC FC kwenye uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa kirafiki kwaajili ya kujiweka vyema na mwendelezo wa ligi kuu kwa upande wa Yanga na ligi daraja la kwanza kwa upande wa KMC FC.
No comments: