Tazama ujazo wa Yanga na dharau zake kwa KMC


MCHEZO wa kirafiki baina ya Yanga SC na KMC ya Kinondoni, utakaofanyika jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam utaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam.
Mkurugenzi wa Michezo wa Azam TV, Patrick Kahemele, mechi hiyo itakayoanza Saa 10:00 jioni itaonyeshwa katika chaneli ya Azam Sports 2.
Yanga inataka kuutumia mchezo huo, kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba Oktoba 14, mwaka huu na KMC ‘inapasha’ kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Kocha Mzambia, George Lwandamina anataka kuwatazama wachezaji wake wengi wa akiba katika mchezo huo, kufuatia nyota wake kadhaa wa kikosi cha kwanza na timu ya taifa ya Tanzania jana kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.
Tanzania na Malawi jana zimetoka sare ya kufungana 1-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Malawi walitangulia kwa bao zuri la Nahodha wake, Robert Ng’ambi dakika ya 35 aliyefunga kwa kichwa cha umbali wa mita 17, kabla ya Winga Simon Msuva kuisawazishia Tanzania kwa kona maridadi kutoka upande wa kulia iliyoingia moja kwa moja byavuni.
Tanzania ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili mechi hiyo baada ya refa Israel Nkongo kuwatoa Erasto Edward Nyoni alitolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kwenda kumpiga mchezaji wa Malawi, Mbulu Richard na kiungo Muzamil Yassin baada ya kumchezea rafu Phiri Gerald.

No comments: