Kiungo wa Yanga, Pappy Tshishimbi alionyesha mapenzi makubwa wakati akimkaribisha kiungo wa pembeni wa Taifa Stars, Simon Msuva.
Msuva anayekipiga Difaa Al Jadid ya Morocco yuko katika kikosi cha Taifa Stars na walikuwa Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi.
Baada ya mazoezi ya Stars, Yanga nao walikuwa wanajiandaa kuanza mazoezi.
Msuva alikwenda kuwasalimia wachezaji wenzake na Tshishimbi alimpokea kwa shangwe kubwa utafikiri watu waliowahi kuwa pamoja.
Wawili hao walizungumza kwa muda na baada ya hapo, Msuva aliendelea kuwasalimia makocha na wachezaji wengine wa Yanga.
No comments: