Mfalme wa Zulu aunga mkono adhabu ya kiboko shuleni


Mfalme wa Zulu Goodwill Zwelithini, amesema kuwa kuondolewa kwa adhabu wa kiboko shuleni, imechangia kuwepo utovu wa nidhamu katika taasisi za masomo.
Alitoa matamshi hayo siku ya Jumanne kwenye mkutano na walimu wakuu wa shule na wasimamizi uliofanyika huko kaskakaizni mwa KwaZulu-Natal
Mfalme Zwelithini ambaye pia ni kinara wa elimu eneo hilo amesema kuwa adhabu ya kibokoa ilichangia wanafunzi kufanya vyema.
"Hiki kitu cha kutowaadhibu watoto wetu kimetuletea madhara kwa sababu watoto hawana nidhamu." alisema mfalme.
Magufuli: Wasichana wanaojifungua hawatarudi shuleni
Adhabu ya kiboko shuleni nchini Afrika Kusini ilipigwa marufuku mwaka 1997. Hata hivyo inaendelea kwenye shule zingine zinazakiuka sheria hiyo.
Mwezi uliopita video ya mwalimu akimchapa viboko mwanafunzi ilisambaa pakubwa katika mitandao ya kijamii.
Mamlaka ziliahidi kumchukulia hatua kali mwalimu huyo.
Pia mfalme amelaani kuuliwa kwa kupigw risasi mwalimu kwenye mkoa wa Guateng, ambao ni kitovu cha uchumi wa Afrika Kusini.

No comments: