Huu ndio uwanja utakaochezwa mchezo wa Simba na Yanga Oktoba 28


KUELEKEA mchezo wa Yanga dhidi ya Simba unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu, hatimaye Bodi ya Ligi imefunguka juu ya uwanja upi ambao utatumika kwa ajili ya mchezo huo.
Timu hizo zitakutana katika mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom ambapo umekuwa na kawaida ya kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa lakini kwa kuwa kwa sasa uwanja huo unafanyiwa marekebisho na hauwezi kutumika hadi miezi mitatu ijayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kuwa Yanga waliandika barua kwenda TFF wakiomba mchezo wao dhidi ya Simba ubadilishiwe uwanja na usiwe wa Uhuru ambao unatumika kwa sasa ukiwa ni uwanja wao wa nyumbani.
Wambura amesema kuwa wamekataa maombi hayo na hivyo mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaama kama ilivyopangwa kutokana na kuwa unakidhi vigezo vya kutumiwa katika mchezo huo ambao huwa unakawaida ya kuwa na upinzani mkali.

No comments: