Dar es Salaam. Kamati ya kusimamia mchakato wa zabuni ya klabu ya Simba, imeandaa mwaliko wa awali kwa ajili ya wanachana na taasisi zenye nia na sifa za kushiriki katika mchakato wa zabuni.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema nyaraka za mwaliko wa awali zipo tayari na wawekezaji kwenye sifa na vigezo wanaweza kuzipata.
"Mwaliko wa kuchukua nyaraka hizi, utatangazwa kupitia vyombo vya habari kwa siku kumi ili kuwapatia fursa za kutosha wazabuni watarajiwa kujiandaa na kukamilisha nyaraka muhimu.
Pia wazabuni watatumia muda huo kufanya mashariano kabla ya kuwasilisha Oktoba 18 ndiyo itakuwa Siku ya mwisho ya kuwasilisha nia ya kushiriki katika mchakato wa uwezekaji.
Alisema hatua hii itafuatiwa na uchambuzi wa mawasilisho yatakayopokelewa ila kutambua wzabuni watakao kuwa wamekidhi sifa na vigezo. Mauzo ya hisa Simba yanukia
No comments: