Hii ndio taarifa kamili juu ya hali ya Amisi tambwe

Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe yuko fiti baada ya kupona majeraha yake na amerejea kwenye kikosi cha Yanga kinachojiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom msunguuko wa sita dhidi ya Kagera Sugar.


Tambwe amekuwa nje wa zaidi ya wiki nane akisumbuliwa na goti ambalo alilitonesha siku moja kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
Kurejea kwa Tambwe kumepunguza presha kwa kocha George Lwandamina kwani tayari alikuwa ameshampoteza mshambuliaji wake mwingine muhimu Donald Ngoma anayesumbuliwa na matatizo ya misuli.
Hata hivyo Daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu amesema Ngoma atarejea dimbani baada ya siku saba hivyo atauwahi mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Tambwe anatarajiwa kurejesha mabao ya Yanga yaliyopotea siku za hivi karibuni!

No comments: