Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT Wazalend,o Zitto Kabwe ameachiliwa huru siku moja baada ya kukamatwa kwake.
Akizungumza na BBC, muda mfupi baada ya kuachiwa, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini, amesema ameachiwa huru baada ya kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka.
Baada ya kujibu mashtaka yaliyomsababishia kufika hapo, aliruhusiwa kuondoka na kuwa huru, huku ikisubiriwa hatua inayofuata ya maamuzi.
Aliitwa na kamati hiyo ya bunge kuhojiwa, kutokana na tuhuma za kudharau bunge na Spika.
Alikamatwa na polisi, siku ya Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, akitokea Kigoma, kutokana na agizo la Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.
No comments: