Katibu wa Machinga soko la Mwenge Bw. Ridhiwani Kimaro amethibitisha kuwa zoezi hilo linaendelea vyema na wafanyabiashara wadogo wanajitokeza kwa wingi kwaajili ya usajili.
Kimaro amesema tayari awamu ya kwanza ambayo ilikuwa ni kutoa elimu imeshafanyika ikifuatiwa na awamu ya pili ambayo ni kupiga picha kwaajili ya vitambulisho na sasa wapo katika awamu ya tatu ambayo ni Machinga waliopiga picha kuchukua Vitambulisho vyao.
Kwa upande wa Machinga wakiwakilishwa na Joseph muuza mitumba amesema wamefurahiswa na hatua hiyo kwani itawanufaisha kwa kutambulika na kufanya kazi zao kwa uhuru bila bugudha walizokuwa wanapata awali lakini pia watafaidika na mikopo ya Ujasiriamali kwasababu watakuwa wanatambulika.
Utaratibu wa kuwasajili Machinga umekuja kufuatia agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli, mapema mwaka huu jijini Mwanza. Rais aliagiza Machinga wasajiliwe ili watambulike na wafanye biashara kwa uhuru
Related posts
Usajili wa machinga waanza
Reviewed by Informalblogsport
on
12:33
Rating: 5
No comments: