Ongeza kipato kwa kutengeneza siagi ya karanga (peanut butter)

Image result for peanut butter IMAGES
Ni vizuri kutafuta na kujifunza njia mbalimbali zinazoweza kusaidia kuboresha uzalishaji wako na pato likawa la uhakika zaidi, ambapo badala ya kuuza karanga zikiwa mbichi. Unaweza kutengeneza siagi ya karanga ukauza ikiwa bidhaa kamili.

Namna ya kutengeneza siagi ya karanga “Peanut butter”
  • Chambua karanga kuhakikisha zote ni nzuri.
  • Kaanga, menya na upepete.
  • Pima uzito kisha saga mpaka ziwe laini.
  • Andaa sukari, chumvi na mafuta ya alizeti.
  • Mafuta yawe 20% ya uzito wa karanga, sukari 6% na chumvi 1.7%.
  • Anza kuweka sukari na chumvi huku ukiongeza mafuta kidogo kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
  • Bandika jikoni moto ukiwa kidogo kwa muda wa dakika kumi na tano.
  • Baada ya muda huo weka kwenye vifungashio na kuweka nembo tayari kwa kupeleka sokoni.


Kama una mtaji mzuri unaweza kuanzisha  kiwanda na kufanikiwa zaidi kwa mashine za kusaga karanga na kutengeneza peanut butter zinauzwa kama 1.8milioni hivyo kuongeza uzalishaji kwa haraka.
mashine ya kutengeneza peanut butter..

No comments: