Producer Mr. T Touch amefunguka jinsi anavyofanya kazi na Young Dee pamoja na Q Boy Msafi
Mr. T Touch ambaye ametengeneza ngoma za Young Dee Bongo Bahati Mbaya na Kiutani Utani ameiambia 5Selekt ya EATV kuwa Dee ndiye mwenye mkataba naye kwa upande wa production ila Q Boy anafanya naye kazi kama wasanii wengine.
“Q Boy ni kama mwanetu ambaye tunaweza tukafanya naye kitu chochote kinachohitajika kufanyika. Hapana, sina mkataba naye kama ilivyo Young Dee ila ni mtu ambaye naweza nikafanya naye kazi,” amesema Mr. T.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa yeye akiwa kama msimamizi wa Young Dee kuna makubaliano kati yake na Q Boy Msafi kwa ajili ya ku-design mavazi ya Young Dee.
No comments: