Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi
Hatua ya kwanza
Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki.
Hatua ya pili
Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke.
Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa.
Hatua ya tatu
Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi.
Njia ya pili
Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C
Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo.
Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya kasha la mbao lilotangulizwa karatasi nyembamba la plastiki subiri saa 3 na sawazisha sabuni kwa rula au kitu kingine kilicho nyooka huku ukigandamiza juu, ipanguse iwe laini kwa kutumia kitamba kilicho lowanishwa.
Katakata sabuni vipande kwa kipimo cha kuuza iweke ikauke katika sehemu yenye kivuli kwa muda wa majuma 8 hadi 12 mfano- ndani ya chumba kwenye sakafu iliyotandikwa kasha la karatasi nene.
No comments: