Wapo watu katika safari ya maisha ambao wapo tayari kukusaidia kukua kimafanikio na kukuona wewe ukifanikiwa na pia wapo watu katika safari ya maisha ambao wao wapo tayari kukuona wewe ukikamwa na hawapendi sana ufanikiwe.
Unapokuwa na kundi kubwa la watu hasa hili la pili ambalo halitaki kukuona wewe ukifanikiwa kwenye maisha yako, uelewe kabisa unakuwa upo katika hatari kubwa sana ya kutokufanikiwa kwa kile ukifanyacho.
Nasema hivyo kwa sababu, watu hawa wanakuwa wanatumia njia au mbinu zao kuhakikisha unakwama au husogei kabisa, yaani wanataka uwe kama wao. Je, watu hawa wanakurudisha vipi nyuma kwenye maisha yako?
1. Kukukosoa sana.
Watu wenye lengo la kukurudisha nyuma, moja ya njia au mbinu wanayoitumia ni kukosoa sana. kila wakati watajaribu kukuonyesha kwamba wewe ni mtu wa kukosea na hadi ujione hufai. Kwa mbinu hii ukiikubali hutafanya kitu, zaidi utatulia usifanye kitu kwa kuogopa kukosolewa.
2. Kutokuthamini mchango wako.
Njia nyingine ambayo watu wenye lengo la kukurudisha nyuma kwenye maisha huitumia sana ni kutokujali mchango wako kabisa. Kila utakachokifanya kitaonekana kwao hakuna kitu. Sasa kwa kuwa umejua hili usijisikie vibaya, kama kuna kitu umekifanya wewe endelea kukifanya kwa moyo wote kwa sababu unajua ni nini ukifanyacho.
3. Kukufanya ujitilie shaka.
Kati ya kitu ambacho hutakiwi kukiruhusu kwenye maisha yako ni kumruhusu mtu mwingine akushushe au akutilie shaka ule uwezo wako mkubwa ulionao. Watu wanaotaka kukurudisha nyuma mara nyingi hutumia mbinu ya kutaka kukufanya ujione huwezi kitu yaani wewe ni mtu wa kawaida tu. Ukiruhusu hali hii utakwama.
4. Kutaka kukufanya ujione maisha yako yamekwama kabisa.
Mbali na kukukosoa sana, kutokukuthamini mchango wako na kukufanya ujitilie shaka, pia watu wanaokurudisha nyuma wanataka wakuonyeshe maisha yako yamekwama kabisa na hakuna njia mbadala ya kuweza kutoka hapo. Hapo watakuonyesha kwamba wewe huwezi kitu.
Hivi ndivyo watu wanavyoweza kukurudisha nyuma kwenye maisha yako ikiwa utawaruhusu kufanya hivyo. Kitu cha msingi ni kuwa makini na njia zao hizo na kuepuka kuendana kama wao wanavyotaka iwe.

No comments: