Msanii wa Bongo Flava, Quick Racka amefunguka sababu za kumtumia Jacqueline Wolper kama video queen katika ngoma yake mpya ‘Still’.
Rapper huyo ambaye amekuwa akibadilika kila wakati katika muziki wake ameiambia 5Selekt ya EATV kuwa wao ni marafiki wa muda mrefu na alitaka mtu ambaye atajiachia ipasavyo.
“Mimi na Wolper tumefanya kazi miaka mingi, ni mshikaji wangu wa miaka mingi na every time tukikutana, tukiwa tunapiga stori, tunafanya kazi huwa tuna vibe na wakati na nafanya video ya Still nilikuwa nataka mtu ambaye atajiachia siyo unaanza kunisimulia unyamwezi,” amesema Quick.
“Wolper ukimwambia nataka ufanye hivi shughuli imesha hiyo, haina haja ya kumuelekeza vitu vingi anajua anachokifanya, so it was it” ameongeza.
Still ni video ya tatu kwa Jacqueline Wolper kutokelezea kwa mwaka huu baada ya Niambie ya Harmonize na Wale Wale ya Shetta.
No comments: