Je, uko tayari kufanikiwa kwa namna yoyote ile? Je, kuna changamoto unazopitia na zinakuzuia kufanikiwa, ingawa wewe kiu yako ni kutaka kuona mafanikio yakiwa kwenye maisha yako? Endapo utamuuliza mtu yeyote swali hili, wengi sana watakwambia, ndio wanataka kufanikiwa, tena utajibiwa kwa haraka sana.
Lakini hata hivyo ni kweli, karibu kila mtu katika maisha yake ana kiu ya kufanikiwa lakini si kila mtu anajua jinsi ya kufanya ili kufanikiwa. Kuna vitabu vingi vimeandikiwa, na makala nyingi zimeandikwa zikieleza kwa wazi nini unapaswa kufanya ili kufanikiwa, na nini ambacho unatakiwa kuepuka sana ili kufanikiwa.
Pamoja na wingi wote wa vitabu na makala hizo za mafanikio, lakini bado watu hawafanikiwi, wamekuwa ni watu wa maisha yale yale, mpaka unaweza ukaa chini ukajiuliza hivi, shida kubwa ipo wapi? Leo kupitia makala haya, nataka nikukumbushe kwa kifupi sana, baadhi ya tabia unazotakiwa uziweke pembeni ili ufanikiwe.
Zifuatazo ni baadhi ya tabia ambazo
1. Ubinafsi.
Sumu mojawapo kubwa katika biashara na mafanikio kwa ujumla ni ubinafsi. Haitakiwi kuwa mbinafsi unapokuwa kwenye biashara, inatakiwa kutoa ushirikiano na kwa wengine ili mafanikio yako ya kibiashara yaweze kukua. Ukiwa mbinafsi, utakosa ushirikiano kwa wengine na utakwama.
2. Hofu.
Hutaweza pia kufanikiwa kama kila wakati kama una hofu kubwa kwenye kila kitu unachotaka kukifanya. Hofu zako zote ulizonazo, zitupe kule. Hofu ni sumu na kizuizi kikubwa sana cha mafanikio yako. Hata hivyo kila mtu ana hofu, lakini hofu zako pia unatakiwa kuzishinda hadi kuchukua hatua kwenye ndoto zako.
3. Uvivu
Je, umeshawahi kukutokea asubuhi ambapo kunapokucha unakuwa unajishauri uamke au usiamke, ndani yako kuna kuwa na mabishano mengi sana ya nini ufanye? Kama hali hiyo ilishawahi kukutokea basi ni dalili mojawapo ya uvivu, ambapo ni kitu kimojawapo unachotakiwa kukitupa kule ili uweze kufanikiwa.
4. Hisia hasi.
Kuendelea kuwa na hisia hasi, wakati unatafuta mafanikio, huko ni kujitafutia balaa la kushindwa kwenye maisha yako. Hisia hasi ni mbaya katika biashara yako, hisia hasi ni mbaya katika maisha yako pia. Zinakufanya ushindwe kufanya mambo yako kwa ufasaha nakujiona kuwa ni mtu kama wa visasi, ziepuke hisia hizi ili ufanikiwe.
5. Waepuke watu hasi sana.
Kama unataka kuwa na mafanikio, epuka sana watu hasi, watu ambao wanaweza kuwa sumu kubwa kwenye maisha yako. Watu hawa hawawezi kukusaidia kitu chochote zaidi watakurudisha nyuma kutokana na maneno yao, kutokana na hisia zao. Wakimbie watu hawa ili utengeneze mafanikio yako.

No comments: